top of page

Mwili Wangu
Ni
Mwili Wangu

Bure Muziki Kuzuia Watoto Kuzuia Programu

Wimbo wa Tatu  Tutacheza mchezo wa “nini iwapo”

Lengo la Wimbo
Kuwafunza watoto kusema HAPANA kwa adhama.

Mchezo wa “nini iwapo” unaweza kutumika katika hali yoyote unayoshuku huenda inamtendekea mtoto. Utumie mchezo huo kuwapa watoto majibu ya hali ngumu ambazo huenda wakashindwa jinsi ya kukabiliana nazo kwa njia salama.
 

Mifano:
1.“Nini Iwapo” mtu atabisha mlangoni na uko nyumbani peke yako?

     a) usiufungue mlango kamwe
     b) iwapo hawataondoka, mpigie simu jirani au jamaa zako.
     c) wapigie polisi simu iwapo huwezi kupata usaidizi wowote na unahofia.

 

2. “Nini Iwapo” mlezi atajaribu kukushika sehemu zako za siri.


       a) Waambie HAPANA kisha nenda kamwambie mtu
       b) Usiliweke jambo hilo kama siri licha ya kuwa atakusihi

 

3. “Nini Iwapo” mtu usiyemjua atakuambia kuwa amempoteza mbwa wake na kuwa
angetaka umsaidie kumtafuta


     a)Mwambie HAPANA na kuwa ulikatazwa kuenda popote na mtu usiyemjua.
        Hata wakisisitiza kuwa wanahitaji usaidizi – ni lazima useme Hapana!

 

Kuwaelezea watoto kuhusu watu wasiowajuaa.

Ukiuliza kikundi cha watoto mgeni ni nani- huenda ukapata majibu 20 tofauti kama vile:

1) ni mtu mbaya

2) ni mtu ambaye atakuumiza

3) ni mtu ambaye hukupa peremende


Huwa tunawafunza watoto wetu:

“usizungumze na wageni”

“usiingie kwenye gari pamoja na mgeni”

“Usikubali peremende kutoka kwa mgeni” 

Lakini…wakati mwingi huwa tunasahau kuwaeleza mgeni ni nani.

Hivyo basi, kwanza tunastahili kuwafunza mgeni ni nani?
Mgeni ni mtu yeyote ambaye hatumjui!
Mgeni huenda akawa:

Mwanaume au mwanamke, mtu mzee au kijana, huenda wakawa tajiri au maskini au mtu wa jinsia yoyote

Bila shaka tunastahili kuwajulisha kuwa sio wageni wote ambao huwa watu wabaya… na endapo mtu umpendaye ama uliye na imani naye atamjulisha mgeni kwako, mgeni huyo huenda mkawa na urafiki naye. Lakini… endapo hukumjua mgeni huyo kupitia kwa mtu umpendaye ama uliye na Imani naye, kamwe hufai kuzungumza naye ukiwa peke yako.

 

Nakala ya Cynthie kutoka kwenye video

Sasa tutacheza mcheza wa “nini kama” na katika wimbo huu tutasoma cha kufanya iwapo mgeni atajaribu kukufanya uende naye, ama kama mtu atajaribu kushika sehemu zako za siri. Je unajua sehemu zako za siri ziko wapi? Ziko sehemu ambayo nguo zako za ndani hufunika. Hakuna mtu anayefaa kuzishika sehemu zako za siri acha tu wakati wewe ni mchanga sana, baba ama mama atakuosha hapo, lakini punde utajua kujiosha mwenyewe. Ama labda wewe ni mgonjwa, Baba ama Mama ama Daktari huenda akakupaka dawa hapo, lakini mbali na hayo hakuna mtu anayefaa kuwa akizishika sehemu zako za siri.

Pia tutasoma cha kufanya iwapo mtu wa familia yenu ama nyumbani kwenu atakufanya upatwe na wasiwasi ama ajaribu kukuumiza. Kila unachofaa kufanya katika mchezo huu ni kukataa kwa sauti “hapana” kwa hivyo nataka useme vizuri kwa sauti

Tutacheza mchezo wa “nini iwapo”

Tutacheza mchezo wa “nini iwapo”
Kuna maswali na majibu kwenu

Kama unataka kuwa mshindi kila wakati
Unafaa kufanya hivi

Sema hapana! Sema tu Hapana!

Nini iwapo, baada ya shule

Mgeni ajaribu kukupeleka nyumbani

Na anaendesha gari jipya linalo meremeta
Na kusema “Hujambo! Unataka kupanda?”
Hapana, wewe ni mgeni

Sitaki kulipanda gari lako

Kwa sababu Mama na Baba yangu waliniambia
Kamwe nisiende na mtu ambaye simjui,
Ningesema hapana!!
Sema tu Hapana!!

 

Sasa nini iwapo, uko nyumbani

Na yaya wanaokuchunga

Na wajaribu kukugusa chini ya nguo zako Ungefanya nini?

Ungesema hapana, yaya

Sitaki ukinigusa hapo

Juu hizo ni sehemu zangu za siri

Na mwili wangu sio mali yako, ningesema hapana!!
Nitasema tu Hapana!!

Tunacheza mchezo wa “nini iwapo”

Kuna maswali na majibu kwenu

Kama unataka kuwa mshindi kila wakati Unafaa kufanya hivi,
Sema Hapana!
Sema tu Hapana!

 

Sasa nini iwapo, kuna mtu

Rafiki ama mmoja wa familia yako

Na hukugusa ama kukuumiza

hukufanya uhisi vibaya ama upatwe na wasiwasi ungesema nini?

Ungesema hapana?

Tafadhali usifanye hivyo

Sipendi ukinigusa hivyo na ingawa nakupenda sana

Tafadhali kuwa mpole na mimi

Juu mimi ni mdogo tu, unaona

Nigesema hapana! Sema tu Hapana!

Sema Hapana!

Nakala hii imeandikwa na kuhuishwa na 

Chrissy Sykes © 2017

Tafsiri : JB Mugi

bottom of page